GISSA Institue Academy

GISSA Institue Academy ✓Daycare and Nursery
✓English Course
✓Pre Form One course
✓Tuition for Primary & Secondary Good care for children and high academic performance

03/01/2025

GISSA ABC DAYCARE AND NURSERY SCHOOL

Tupo TANGA-Korogwe mji
Contact: 0719468583/0622762837

03/01/2025
03/01/2025
GISSA ABC DAYCARE AND NURSERY SCHOOLHabari walezi wenzangu,?Tunatumai muwazima wa Afya🌹Naamini sote tunayo taarifa ya *u...
22/08/2024

GISSA ABC DAYCARE AND NURSERY SCHOOL

Habari walezi wenzangu,?
Tunatumai muwazima wa Afya🌹

Naamini sote tunayo taarifa ya *ugonjwa mpya* wa _virusi vya homa ya nyani_ (monkey pox), Muhimu tuchukue tahadhari.

Ila...!
MAGONJWA YANA NJIA ZAKE ZA KUAMBUKIZA! hili tunalifahamu,

Na njia zote za uambukizi zimeelezewa kisayansi, na sote tunakubali kuwa sayansi bado haijafikia kikomo na haiwezi kuwa na ukomo abadan!

I mean, kuna baadhi ya njia za uambukizi wa magonjwa bado hazijagundulika mpaka sasa na kuna uwezekano hata zikigundulika itachukua muda sana majibu yake kuyathibitisha kisayansi zaidi, Sio kwa sababu ya kukosekana kwa elimu, laa zipo sababu nyingi zinazopelekea kutokuonekana na kugundulika kwa njia hizi mpya za uambukizi kisayansi

Magonjwa ya siku hizi yamekuwa ya kutengenezwa, kwa hivyo hutengenezwa ugonjwa ukiwa na chanjo au dawa yake, ila watengenezaji huanza kutangaza ugonjwa na kuacha ugonjwa uenee kisha baadae kutangaza nhanjo au tiba yake!

Hivi ni kawaida sana, na mbinu hizi hutumiwa na mataifa makubwa upande wa siasa za nje kwa mataifa mengine, ni silaha zao za kutishia ulimwengu juu ya ubwana wao na ukubwa wao, na ni njia za kujilinda dhidi ya maadui zao!

Muhimu juu yetu k**a familia ya GISSA ni kuzingatia yafuatayo
1. Tuepuke kuwekeza hisia kubwa juu maono ya ugonjwa husika au matokeo ya ugonjwa na madhara yake, hii ni hatari sana kwa afya ya akili na mwili, mwili una tabia ya kuleta mwitikio (response ) kwa kila hisia inayotua juu ubongo! Hali hii inaweza kuleta mshtuko kwenye kinga ya mwili na kusababisha kushuka kwa kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa husika, ni mfano wa stress ama uoga namna unavyokula kinga ya mwili kwa haraka na kukosa uwezo wa mwili kujilinda, hivyo tupunguze kukithirisha kuangalia na kutuma picha zinazoonesha ukwasi wa madhara ya ugonjwa husika, ni hatari mno, tuepuke kuwaonesha *watoto wadogo na wachanga* picha za namna hii (mfano hiyo hapo juu) ni muhimu hapa kunielewa hata k**a sijatoa sababu, inawezekana sababu ikawa ni upendo juu ya watoto wetu kwasababu ni jukumu letu kuwalea, kuwalinda na kuwahidumia!

2. Tusiwekeze imani kubwa juu ya kasoro zenye kutia wasiwasi juu kuupata ugonjwa husika kwa haraka, ni hatari pia kwa mhusika wa imani hii, badala yake tuwekeze imani zetu kubwa juu ya kutokufikiwa na ugonjwa husika huku tukiweka imani kubwa juu ya MUUMBA kuwa atatusitiri, atatulinda na kutuweka mbali dhidi ya gonjwa hili hatari na mengineyo.

Miongoni mwa kanuni ndogo za kisaikojia ni kuwa " *matendo ya mwanadamu yapo juu ya dhana yake"* hii ni sawa na yule aliesema " aliwazalo mjinga ndilo litakalomtokea" basi tufanye kinyume chake tutapata majibu halisi kwanini tunashauri kupunguza misingo juu ya magonjwa haya hatari hasa ya kuzuka,
ila muhimu tuamini sote kuwa hakuna ugonjwa usio na dawa!

3. Tusife moyo juu ya chochote kinacho tokea hasa kwenye maisha hadi (or in negative way), ikiwa ni ugonjwa, ajali , kupotelewa na mengineyo, Daima tuamini tutashinda, sayansi haitaki kukubali uwepo M/M/MUNGU ila ajabu hakuna mwanadamu aliyekiri kujiumba mwenyewe!
Imani yetu ni kuwa "MUNGU aliumba dawa na hakuumba ugonjwa, tunaamini tutapita katika hili kwa Qudra zake, Maisha ya mwanadamu ni hadithi fupi tu ya kusimuliwa hapa ulimwenguni, alisema mzee mwinyi 😂 👍

Tutashinda kwa pamoja tukimtegemea M/MUNGU,
*GISSA ABC DAYCARE*
KOROGWE-MANUNDU,

Sambaza kwa wengine,
Muwe siku NJEMA!💪🌹

Address

Children Learn Better In A Free Fear Environment
Tanga

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when GISSA Institue Academy posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to GISSA Institue Academy:

Share