28/05/2025
Inaelezwa kuwa Young Africans Sports Club walishamaliza kufanya usajili wa wachezaji wote wanaowahitaji kuelekea msimu ujao 👀
Mchezaji ambaye wamechelewa kukamilisha mazungumzo alikuwa ni Komizo Abdoul Abass Maiga 🇨🇮 .
Kuhusu kiungo huyo wa kati wa ASEC Mimosas ni kwamba, tayari Yanga wamekamilisha taratibu zote kwa kushirikiana na wakala wa mchezaji; hivyo Koimizo Maiga yupo tayari kucheza Young Africans sc msimu wa 2025-2026.
Mimi binafsi nimechelewa sana kuujua uwezo wake. Nilisikia kuwa amepata malezi yake ya soka nchini Ufaransa kwenye Academy ya ASSE - Association Sportive de Saint-Etienne 🇫🇷 Nikaenda kujiridhisha.