Dar Rapid Transit Agency - DART

Dar Rapid Transit Agency - DART Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Dar Rapid Transit Agency - DART, Cargo and freight company, Kariakoo.

DART Agency operates under the Prime Minister’s Office, Regional Administration and Local Government through the Ministerial Advisory Board to establish and operate Bus Rapid Transit (BRT) in Dar es Salaam City.

19/01/2019

Matokeo makubwa sasa/Big Results Now iling'oka na JK ingawa watendeji wengi bado wapo serikalini. Like parrots the same guys are now singing "Tanzania ya Viwanda" hahaha! Ikitokea akaja mwingine akawaimbisha "Tanzania ya Wajanja" wataimba tu bila kuhoji! I love this country, I hate Tanzanian hypocrites!

MATOKEO MAKUBWA SASA: Mtendaji Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo akijadili jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa...
21/09/2013

MATOKEO MAKUBWA SASA: Mtendaji Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo akijadili jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa na viongozi wengine wa Halmashauri ya Manispaa ya Kindondoni baada ya ufunguzi wa mkutano. Anaonekana akiwaambia kuwa DART ni moja ya miradi iliyo katika mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).

TUNATAMBUA MCHANGO WA WAMILIKI: Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mh. Dkt. Didas Masaburi akisisitiza umuhimu wa k...
21/09/2013

TUNATAMBUA MCHANGO WA WAMILIKI: Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mh. Dkt. Didas Masaburi akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wamiliki wa daladala katika uendeshaki wa mfumo wa DART wakati akibadilishana mawazo na mmoja wa wadau walioshiriki katika mkutano huu.

TUNAFUATILIA: Wamiliki wa Daladala wakifuatilia mawasilisho ya mada kwa umakini. Mkutano huu ulihusu pamoja na mambo men...
21/09/2013

TUNAFUATILIA: Wamiliki wa Daladala wakifuatilia mawasilisho ya mada kwa umakini. Mkutano huu ulihusu pamoja na mambo mengine, namna wamiliki wa Daladala wanaweza kushiriki katika uboreshaji wa mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka ikiwa ni pamoja na fursa zitakazotokana na mfumo huo.

NAFUNGUA MKUTANO: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said M. Sadik akifungua mkutano wa pamoja kati ya Wakala wa Mabasi ...
21/09/2013

NAFUNGUA MKUTANO: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said M. Sadik akifungua mkutano wa pamoja kati ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Wamiliki wa Daladala katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam hivi majuzi.

FURSA: Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Jijini Dar es Salaam (DART) umeandaa mkutano wa pamoja na wamiliki wa magari ya ...
12/09/2013

FURSA: Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Jijini Dar es Salaam (DART) umeandaa mkutano wa pamoja na wamiliki wa magari ya daladala katika Jiji la Dar es Salaam ili kuwafahamisha wamiliki hao FURSA za uwekezaji katika mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART). Mkutano huu utafunguliwa na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Meck Sadik na utafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere siku ya Alhamisi terehe 19 Septemba, 2013 Tafadhali wadau sambazeni ujumbe huu ili watu wachangamkie fursa hizi...

TUNAHITAJI KUBADILIKA....
09/09/2013

TUNAHITAJI KUBADILIKA....

...na sisi tunavunja sheria pia!
09/09/2013

...na sisi tunavunja sheria pia!

...biashara zinaendelea!
09/09/2013

...biashara zinaendelea!

TUNAVUNJA SHERIA: Wafanyabiashara wadogo wadogo wakiendelea na biashara zao katika maeneo ya miundombinu ya DART eneo la...
09/09/2013

TUNAVUNJA SHERIA: Wafanyabiashara wadogo wadogo wakiendelea na biashara zao katika maeneo ya miundombinu ya DART eneo la Manzese Midizini na kukaidi tangazo la kuwataka kuondoka lililotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni tangu juzi ijumaa mpaka jana Jumapili tarehe 8/9/13. Manispaa ya Kinondoni wakishirikiana na DART wanawataka wafanyabiashara hawa kuacha kufanya hivyo ili kumpisha mkandarasi kuendelea na kazi yake ya ujenzi bila bugudha. Ndugu wadau nini maoni yako kuhusu hili?

04/09/2013

Ndugu wadau na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla napenda kuwajulisha kuwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeweka mkakati kabambe wa kuhakikisha kuwa miundombinu ya DART inalindwa na kutunzwa ili kuepusha uharibifu unaoweza kujitokeza kutokana na shughuli za watu k**a vile biashara ndogo ndogo katika ushoroba (corridor) wa ujenzi wa miundombinu yake. Mkakati huu shirikishi umehusisha wenyeviti, watendaji wote katika kazi za serikali za mitaa na vitongoji pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Lengo la kampeni hii ni kuweka mazingira bora yatakayomuwezesha Mkandarasi kufanya kazi bila bughudha yoyote na hivyo kumaliza kazi ya ujenzi kwa wakati. Ukiwa sehemu muhimu ya ufanikishaji wa lengo hili tunaomba ushiriki wako kwa kuepuka vitendo ambavyo vinaweza kukwamisha adhma hii ikiwa ni pamoja na kuondoa biashara yako bila shuruti katika miundombinu ya DART, kutonunua bidhaa katika maeneo yasiyo rasmi hususan katika miundombinu ya DART, kutokubali kukatiza barabara sehemu isiyostahiki k**a bodaboda nyingi zinavyofanya! Tunaamini kuwa kwa umoja wetu tukiweza kufanya haya tutamwezesha mkandarasi kutekeleza wajibu wake kwa wakati na ufanisi na kuweka mandhari ya Jiji katika hali ya kupendeza na kuvutia. Tunatanguliza Shukrani zetu za dhati kwako mdau.

NAJIBU MASWALI: Waziri wa Nchi, OWM-TAMISEMI, Mh. Hawa Ghasia akijibu maswali ya waandishi wa Habari wakati wa ziara  ya...
01/09/2013

NAJIBU MASWALI: Waziri wa Nchi, OWM-TAMISEMI, Mh. Hawa Ghasia akijibu maswali ya waandishi wa Habari wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge, Kimara Mwisho hivi majuzi.

Address

Kariakoo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dar Rapid Transit Agency - DART posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Dar Rapid Transit Agency - DART:

Shortcuts

Share