05/05/2021
********* KIAZI SUKARI (BEETROOT) ********************
--------------------------------------------------------------------------
Hapo kale, kiazi sukari kilikuwa kinatumika k**a dawa kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali k**a kuvimbiwa, majeraha pamoja na matatizo ya ngozi (ilikuwa ikitumika mizizi)
******AINA ZA BITIRUTI (BEETROOT)*****
Kuna aina mbalimbali za bitiruti k**a vile vyekundu vyenye mistari myeupe kwa ndani, pamoja na nyeupe, hata hivyo bitiruti ndiyo inayolimwa kwa wingi nchini kwetu Tanzania. Aina zote hizi huweza kuliwa majani na mizizi pia. Hata hivyo kutokana na kiwango cha sukari inayopatikana, huwa na ladha zaidi k**a kikiliwa kibichi.
***** MATUMIZI ******
Zao hili lenye madini ya foliate, chuma, magnesiamu, vitamin C na potashiamu lina matumizi mengi kwa binaadamu na hata kwa wanyama.
Bitiruti hutumika k**a chakula au kiungo k**a vile karoti kwa ajili ya kuongeza ladha kwenye vyakula mbalimbali.
Zao hili hutumika kutengenezea juisi. unaweza kutumia bitiruti pekee au ukachanganya na matunda mengine.
Huongeza damu mwilini pamoja na kuupa mwili nguvu na kusaidia kuboresha kumbukumbu.
pia inasadikiwa hutibu ugonjwa wa sukari, kuvimbiwa, majeraha na magonjwa ya ngozi.
Zao hili pia majani yake huweza kutumiwa k**a lishe kwa ajili ya kulishia mifugo wa aina yoyote.
**** HALI YA HEWA *****
Zao hili hufaa zaidi kulimwa katika hali ya baridi kidogo hasa nyuzi joto 18 c hadi 27 c.
***** UDONGO *****
Zao hili hufaa zaidi kulimwa katika udongo wa tifutifu na wenye rutuba ya kutosha (loam soil). Halifai kulima katika udingo wa mfinyanzi. Ikiwa shamba halina rutuba ya kutosha basi ni vyema kuweka mbolea ya mboji katika shamba kabla ya kuotesha.
***** UANDAAJI WA SHAMBA*****
Kutokana na kuwa zao hili huoteshwa au kusiwa moja kwa moja shambani, mkulima ni lazima kuandaa shamba mapema mara tu anapohitaji kupanda.
Ili kurutubisha udongo na kupata mavuno mengi, weka mbolea ya samadi iliyoiva au mboji shambani kabla ya kulima. Hii inasaidia udongo na kuchanganyika vizuri wakati wa kulima.
Tengeneza matuta katika shamba Zima. Kitaalamu, matuta ya kunyanyua ni mazuri zaidi katika kilimo cha kumwagilia hasa kwa zao la bustani k**a hili. Matuta haya husaidia maji kupenya ardhini na kuruhusu mizizi kupata maji ya kutosha huku mmea ukitanuka vizuri na kujitengenezea chakula.
mwagilia matuta kwa kuweka maji ya kutosha, tayari kuotesha siku ya pili. Namna ya kuotesha, kumbuka kuwa kila ekari moja, unaweza kutumia mbegu za bitiruti kiasi cha gramu 50 na kwa kutumia vipimo sahihi utakuwa na jumla ya mimea 108,000
Otesha mbegu katika mistari kwenye matuta huku ukihakikisha kuna nafasi ya kutosha kati ya mstari na mstari na kati ya mche na mche. Baada ya kuotesha mbegu zitachipua baada ya siku 10 (wiki na siku tatu ).
***** NAFASI NA KUMWAGILIA ******
Ni vizuri zaidi ukatengeneza matuta yenye upana wa sentimeta 150 kila moja na katika kila tuta weka mistari mine ya bitiruti.
Nafasi kati ya mche na mche iwe ni sentimeta 10.
mstari na mstari iwe ni sentimeta 15.
Baada ya miche kuchipua, anza kumwagilia katika wiki ya pili. Mwagilia kila wiki mara moja au mbili kulingana na ukavu wa shamba. Zao hili halihitaji maji mengi kwani husababisha fangasi pamoja na kuoza kwa kiazi hivyo usimwagilie kila wakati.
***** PALIZI ******
Ni muhimu kufanya palizi kila mara unapoona majani yanachipua yaani muda wote kuanzia ukuaji hadi kuvuna. Ondoa magugu yakiwa bado machanga kwani zao hili haliwezi kuendelea kwani yana uwezo mdogo sana kushindana na magugu.
******* MAGONJWA NA WADUDU ******
K**a ilivyo kwa mazao mengi ya bustani, zao hili pia hushambuliwa na maginjwa k**a powdery mildew na down mildew.
Aidha, wadudu k**a thiripi, inzi weupe na utitiri pia hushambulia zao hili.
****** NAMNA YA KUZUIA******
Hakikisha unaotesha katika eneo lenye hali ya hewa inayohitajika, isiwe ni kipindi cha mvua nyingi wala usiweke maji mengi.
Ikiwa utatumia viuatilifu, basi hakikisha unapata ushauri kutoka kwa wataalamu wa kilimo.
**** MAVUNO *****
Zao hili hukomaa na kuvunwa baada ya miezi mitatu (siku 90). Hata hivyo huweza kuvumilia kusubiri soko ikiwa mkulima atalazimika kufanya hivyo (huweza kukaa miezi mitatu toka kukomaa bila kuharibika kwa kuvuna na kuhifadhi sehemu yenye ubaridi kiasi).
***** USHAURI ****
Kutokana na matumizi ya zao hili, si vyema kutumia kemikali. Ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo hai ili kulinda afya za walaji.