Aviation Tanzania

Aviation Tanzania A digital media platform delivering trusted insights, perspectives, and stories on the development of the aviation industry locally and globally.

https://whatsapp.com/channel/0029VaG0R8tAe5VzPI8VZL2k
Connecting Aviation Stories, People & Progress

Kwa zaidi ya miongo miwili, shirika binafsi la ndege la Flightlink limekuwa likitoa huduma za usafiri wa anga kwa abiria...
14/09/2026

Kwa zaidi ya miongo miwili, shirika binafsi la ndege la Flightlink limekuwa likitoa huduma za usafiri wa anga kwa abiria ndani ya Tanzania na katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Leo, tuangazie idadi ya ndege zinazotumiwa na shirika hili kwa sasa, pamoja na mpango uliopo wa shirika hili katika kuongeza idadi ya ndege zake.

14/09/2026

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imesherekea ushindi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere ambacho hivi karibuni kimenyakua tuzo ya kimataifa ya World Travel Awards kwa kuandaa bonanza lililowakutanisha wafanyakazi wa TAA na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa anga katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Bonanza hilo lilihusisha michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, kuvuta kamba, mbio za magunia, kukimbiza kuku pamoja na mbio za masafa mafupi na marefu, ikiwa na lengo la kuimarisha afya, umoja, upendo na mshik**ano miongoni mwa washiriki.

Katika bonanza hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Abdul Mombokaleo, amewahimiza wafanyakazi na wadau wa sekta ya usafiri wa anga kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha afya na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema bonanza hilo pia lilikuwa sehemu ya kusherehekea na kupongezana kufuatia JNIA kutwaa tuzo ya kiwanja bora cha ndege Afrika 2026, ushindi ambao umeifanya Tanzania kupokea tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.

Katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika kwenye bonanza, timu ya TAA iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Bi. Irene Minja, amewashukuru wafanyakazi na wadau kwa mchango wao katika kuiwezesha JNIA kutwaa tuzo hiyo, akieleza kuwa bonanza hilo pia limekuwa fursa ya kujenga mahusiano, kuimarisha ushirikiano na kuongeza ari ya kufanya kazi kwa pamoja.

Aidha, TAA imetangaza mpango wa kuanzisha Airport Marathon, itakayowakutanisha wafanyakazi na wadau wa viwanja vya ndege katika shughuli za michezo na mazoezi, huku taasisi nyingine zikialikwa kushirikiana na TAA katika mabonanza na shughuli nyingine za kuimarisha afya na mshik**ano.

Tanzania na Misri zimefanya majadiliano ya namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za ulinzi na teknolojia ya anga,...
14/09/2026

Tanzania na Misri zimefanya majadiliano ya namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za ulinzi na teknolojia ya anga, hususan katika kubadilishana ujuzi, uzoefu na teknolojia kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo yalifanyika katika maonesho ya Kimataifa ya Anga na Teknolojia za Juu (ELIAS) nchini Misri yakimuhusisha Waziri wa Ulinzi na JKT wa Tanzania, Dkt. Rhimo Nyansaho, na Waziri wa Ulinzi na Uzalishaji wa Kijeshi wa Misri, Luteni Jenerali Ashraf Salem Zaher.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili fursa za kuendeleza ushirikiano katika teknolojia za ulinzi na anga, pamoja na maeneo mengine ya teknolojia za kisasa yenye maslahi kwa Tanzania na Misri.

Tanzania ilishiriki maonyesho hayo kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali kwa wadau wa kimataifa, kubadilishana uzoefu na kujenga uhusiano wa kimkakati katika sekta za ulinzi, anga na teknolojia za kisasa.

12/09/2026

Katika mahojiano maalumu na Bi. Neema Mukurasi, Meneja wa jengo jipya la abiria, Uhuru VIP Terminal and Lounge, anaeleza utofauti wa huduma zinazotolewa ndani ya jengo hilo na namna abiria anavyohudumiwa kuanzia anapoingia hadi anapoondoka.

Bi. Neema anaeleza zaidi kuhusu huduma zinazotolewa ndani ya Uhuru VIP Terminal and Lounge, iliyopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, na namna zinavyolenga kuboresha uzoefu wa abiria.

Miracle Concierge | Luxury Airport Hospitality Miracle Air | Luxury Flights Tanzania

Dubai-based airline flydubai is set to launch dedicated cargo operations from October 1, 2026, with three Boeing 737-800...
11/09/2026

Dubai-based airline flydubai is set to launch dedicated cargo operations from October 1, 2026, with three Boeing 737-800 freighter aircraft.

The aircraft will be operated under a wet-lease agreement with SolitAir and will add around 23,000 kilograms of cargo capacity per flight. Unlike the belly-hold cargo carried on passenger aircraft, the freighters will offer dedicated main-deck space for larger shipments.

The new service will increase flydubai’s cargo capacity ahead of the busy fourth-quarter cargo season and is part of the airline’s strategy to expand its cargo business.

Looking ahead, flydubai also plans to use the cargo capacity of its future Boeing 787-9 Dreamliner fleet, with 30 aircraft currently on order. The airline is also considering converting passenger aircraft into freighters from 2029.

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Tanzania Airports Authority inatarajia kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 35 wa Bara...
11/09/2026

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Tanzania Airports Authority inatarajia kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 35 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege Afrika (ACI Africa), unaotarajiwa kufanyika jijini Abuja, nchini Nigeria kuanzia Septemba 19–25, 2026.

Mkutano huo utajadili namna ya kuboresha utendaji wa viwanja vya ndege na kuhakikisha vinaendelea kutoa huduma bora hata wakati wa changamoto.

TAA imesema ushiriki wake utatoa fursa ya kujenga ushirikiano wa kimkakati na kushiriki katika mijadala inayolenga kuimarisha maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga barani Afrika.

Shirika la ndege la Flightlink linatarajia kuongeza ndege mpya nne aina ya Cessna 208B Grand Caravan EX, hatua inayoleng...
10/09/2026

Shirika la ndege la Flightlink linatarajia kuongeza ndege mpya nne aina ya Cessna 208B Grand Caravan EX, hatua inayolenga kuongeza idadi ya ndege zake na kuimarisha huduma kwa abiria katika safari za ndani na za kikanda.

Flightlink imetangaza mpango huo baada ya kusaini makubaliano ya ununuzi wa ndege hizo na kampuni ya Africair,katika Mkutano wa Aviation Africa uliofanyika Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, ndege mbili zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwaka 2026, huku ndege mbili nyingine zikitarajiwa kuwasili katika robo ya tatu ya mwaka 2027.

Mkurugenzi Mtendaji wa Flightlink, Munawer Dhirani, amesema ujio wa ndege hizo ni hatua muhimu katika ukuaji wa shirika hilo na utaongeza uwezo wa kuunganisha maeneo mbalimbali ya utalii Afrika Mashariki.

Kuwasili kwa ndege hizo nne, kutaiwezesha Flightlink kuwa na jumla ya ndege sita aina ya Cessna Grand Caravan EX.

Kenya is hosting the African aviation community for the Aviation Africa Summit, bringing together industry leaders, poli...
10/09/2026

Kenya is hosting the African aviation community for the Aviation Africa Summit, bringing together industry leaders, policymakers, investors and aviation professionals for two days of discussions on the future of aviation across the continent.

The summit was officially opened on 9 September 2026 by Kenya’s Prime Cabinet Secretary, H.E. Musalia Mudavadi, alongside Principal Secretary for Aviation and Aerospace Development, Teresia Mbaika.

Discussions at the summit are focusing on key areas including air connectivity, airport infrastructure, innovation, investment and the growth of Africa’s aviation sector.

The Kenya Airports Authority (KAA) is also participating in the forum, using the summit as an opportunity to engage industry stakeholders, explore partnerships and exchange ideas aimed at advancing airport infrastructure and improving passenger experience.

The summit comes as African countries continue to seek stronger air connectivity and investment to support the growth of aviation and tourism across the continent.

10/09/2026

Ni rasmi sasa, Uhuru VIP Terminal and Lounge, jengo jipya la abiria lililopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), limeanza kutoa huduma kwa wasafiri wanaowasili na kuondoka kupitia uwanja huo.

Ndani ya Uhuru VIP Terminal zinatolewa huduma maalumu (VIP services), K**a vile sehemu za kupumzika, chakula na huduma nyingine zinazomsaidia abiria kuwa na safari rahisi na yenye utulivu.

Je, kuongezeka kwa huduma k**a hizi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kunaleta tija gani kwa sekta ya utalii na usafiri wa anga nchini Tanzania?

Miracle Concierge | Luxury Airport Hospitality  has introduced the Uhuru VIP Terminal at Kilimanjaro International Airpo...
09/09/2026

Miracle Concierge | Luxury Airport Hospitality has introduced the Uhuru VIP Terminal at Kilimanjaro International Airport (KIA), offering travellers a more private, comfortable and seamless airport experience when arriving in, departing from or transiting through Tanzania.

The Uhuru VIP Terminal offers dedicated check-in and luggage handling, immigration and security screening, as well as VIP spaces, premium lounges, private rooms and quiet areas.

Travellers can also access freshly prepared meals and refreshments, with services designed to provide a seamless experience throughout the arrival, departure and transit processes.

Located at the gateway to Tanzania’s northern safari circuit, the facility is designed to enhance the travel experience for visitors heading to the country’s leading safari destinations while contributing to the development of premium airport hospitality in Tanzania.

The Uhuru VIP Terminal is part of Miracle Collection’s commitment to “Elevating Extraordinary Journeys,” with a focus on providing a refined and personalised experience for travellers using Kilimanjaro International Airport.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Aviation Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Aviation Tanzania:

Shortcuts

Share