19/05/2026
Yesterday 18th May 2026, our Board Vice Chairman Mr. Vincent Shirima alongside our Group Managing Director and CEO Mr. Patrick Mwanri, had a great privilege of meeting Hon. Dr. Mwigulu Lameck Nchemba (MP), Prime Minister of The United Republic of Tanzania and Deputy Minister of Transport Hon. David Kihenzile as part of strategic stakeholders engagement initiatives.
During the meeting, Mr. Patrick Mwanri briefed Hon. Prime Minister on the strategic role that Precision Air is playing in supporting national economy especially in Air Transport and Tourism sectors. He also highlighted future strategies that the Airline has in furthering its contribution to the economy.
On his side, Hon. Dr. Mwigulu emphasized the need of continuing involving Private Sector in driving national economy. Promising to continue receiving opinions from private sector and investors in efforts to improve private sector participation and environment in Tanzania.
Jana tarehe 18 Mei 2026, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air, Bw. Vincent Shirima, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Patrick Mwanri, walipata wasaa wa kukutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, pamoja na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kimkakati za kuimarisha ushirikiano na Serekali.
Katika kikao hicho, Bw. Patrick Mwanri alimweleza Mheshimiwa Waziri Mkuu kuhusu mchango wa Precision Air katika kukuza uchumi wa taifa, hususan katika sekta za usafiri wa anga na utalii. Aidha, alimueleza zaidi juu ya mikakati ya shirika hilo la ndege katika kuendelea kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuhusisha sekta binafsi katika kuendesha uchumi wa taifa. Pia aliahidi kuendelea kupokea maoni kutoka kwa wawekezaji katika jitihada za kuboresha mazingira ya sekta binafsi nchini Tanzania.