Uvitama GROUP

Uvitama GROUP karibu upate huduma za usafiri wa uhakika na
salama

Habari,ni septemba moja leo na nitumaini langu mko sawa,leo naomba kushare nanyi habari hii:-FUNIKA AIBU ZAO BADALA YA K...
01/09/2022

Habari,ni septemba moja leo na nitumaini langu mko sawa,leo naomba kushare nanyi habari hii:-FUNIKA AIBU ZAO BADALA YA KUWAAIBISHA

Baada ya kusafisha na kupanga nyumba yangu, kaka yangu alinipigia simu na kuniambia, "Mimi na mke wangu tunakuja kukutembelea."

Nilienda jikoni kuwaandalia kitu, lakini sikuweza kupata chochote cha kuandaa.

Baada ya kufikiria sana na kupekua, nilichoweza kukiona ni machungwa machache. Kwa hivyo, nilitengeneza vikombe viwili vya juisi baridi mara moja.

Ndugu yangu na mkewe walipofika nilishtuka kumuona akiwa na mama mkwe wake ambaye alikuja kuwatembelea kwa mara ya kwanza.

Kwa hivyo nikatoa vikombe viwili vya juisi kwa mkewe na mama yake, na nikampa kaka yangu kikombe cha maji, nikisema, 'Najua kwamba unapenda Sana Kunywa Sprite.'

Alikunywa kinywaji na akagundua kuwa ni maji ya kawaida, lakini hakusema wala kuonyesha dalili yoyote kuwa yalikuwa maji na si sprite

Na ghafla mama mkwe wake akasema, Nina kiu ya Sprite na kumuomba kaka ampe

Hapa nilishtuka na nikajua ninapata aibu.

Lakini kaka yangu aliniokoa kwa kumwambia, 'nitakuletea glasi yako kutoka jikoni.'

Baada ya muda tulisikia sauti ya glasi ikivunjika jikoni. Kisha akarudi na kumwambia mama mkwe, 'Samahani, iliniponyoka mkononi na glasi ikavunjika. Lakini hakuna shida, nitaenda dukani kukununulia nyingine.

Mkwewe alikataa na kusema, "Hakuna haja haikuwa riziki yangu hata hivyo"

Mwishowe wakati wanaondoka, kaka yangu aliniaga na akanipa pesa mkononi kwa namna ambayo hakuna aliyegundua kuwa nimepewa pesa na kusema, "Usisahau kusafisha ile sprite jikoni sisimizi wasije wakaharibu" Na aliniaga kwa tabasamu na upendo.

Kwa njia hii, kaka yangu alijali hisia zangu na kuficha kasoro yangu. HUU NI UPENDO WA ZAIDI YA NDUGU WA DAMU

Unapokuwa katika nafasi, tumia kuinua wengine. Kumdidimiza mtu yeyote kamwe hakutakufanya uwe bora!

JE! UNAFICHA AIBU ZA WENGINE AU WEWE NDIO NAMBA MOJA KUWATANGAZA NA KUYASEMA VIBAYA MAPUNGUFU YAO?

(Jitazame)

04/09/2021
26/08/2021

Ajali ya sauli

30/04/2021

Karibu katika ukurasa wa UVITAMA GROUP,ni ukurasa unaohusu usafiri na ujasiliamali,.....

feeling the mom's love
18/03/2021

feeling the mom's love

Karibuni,bwana dere anawakaribisha kwa safari za dsm na maeneo ya karibu
17/12/2020

Karibuni,bwana dere anawakaribisha kwa safari za dsm na maeneo ya karibu

16/11/2020

Usafirishaji kwa bajaj mjini,count on us

Address

Tabata Reli
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 06:00 - 23:00
Tuesday 06:00 - 23:00
Wednesday 06:00 - 23:00
Thursday 06:00 - 23:00
Friday 06:00 - 23:00
Saturday 06:00 - 23:00
Sunday 06:00 - 23:00

Telephone

+255736004333

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Uvitama GROUP posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Uvitama GROUP:

Share