Dadani Investment Company Limited

Dadani Investment Company Limited (ii)

(i) To carry on the business of buying and selling real estates, leasing and developing properties, property developers, entering into Joint venture, Partnership, Private Public Partnership for purposes of carrying out property development business.

My President
09/01/2024

My President

Mfariji Mkuu. Karibu Mkoa wa Manyara
07/12/2023

Mfariji Mkuu. Karibu Mkoa wa Manyara

08/05/2023
*ASITOKEE KIONGOZI KUWATISHA WATOA TAARIFA KUPITIA MFUMO WA SNR DK.MWINYI AONYA*Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza...
29/03/2023

*ASITOKEE KIONGOZI KUWATISHA WATOA TAARIFA KUPITIA MFUMO WA SNR DK.MWINYI AONYA*

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka viongozi  wa umma   kuwajibikaji kwa  kero na changamoto wanazowasilishiwa na mfumo wa Sema Na Rais (SNR) .Amesema wapo baadhi ya viongozi  wasiotaka kutatua changamoto hizo kwa vile hawaoni umuhimu wake na akawaonya atawachukulia hatua . Dk.Mwinyi halikadhalika amebainisha kupitia mfumo huo kuna utambuzi wa kitakwimu kujua kiongozi au taasisi zisizofanya vizuri na sasa wakati umefika kila mmoja aone umuhimu wa kuwajibika.

Rais Dk.Mwinyi ameyaeleza hayo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport kwenye kikao kazi  cha maadhimisho ya miaka miwili tangu kitengo cha Sema na Rais Mwinyi (SNR)  kilipoasisiwa .Kitengo hicho kipo chini ya Afisi ya Rais Ikulu.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi akizungumzia  mafanikio ya mfumo wa SNR kwa kipindi hicho cha miaka miwili alisema mfumo huo umeleta tija kwa wananchi ambao changamoto zao zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa na mfumo ataendelea kuusimamia vema.

Alizungumzia pia suala la taarifa za ubadhirifu wa mali za umma na akaonya asitokee Kiongozi yeyote kuwatisha wanaowasilisha kero au changamoto kupitia mfumo wa SNR na akaahidi hatua zitachukuliwa dhidi ya kiongozi huyo. Ameahidi mtoa taarifa atalindwa na kuwaambia maafisa wa SNR wafanye kazi zao bila woga.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi alieleza kuthamini uhuru wa Mahakama na Serikali itayafikisha mbele ya haki matatizo yatakayopelekwa na SNR Mahakamani kwa Jaji Mkuu ayashughulikie na kuondoa kasoro zinazojitokeza .Katika msingi wa utawala bora Mheshimiwa Rais alibainisha Serikali haina haki kuingilia mhimili wa Mahakama ila ina wajibu kuwasilisha changamoto wazishughulikie.

📅 29 Machi, 2023

📍Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

*RAIS DK.MWINYI  AWASILI DAR KUHUDHURIA UZINDUZI WA JUKWAA LA MTANDAO WA CHAKULA AFRIKA, AGRF 2023* Rais wa Zanzibar na ...
17/03/2023

*RAIS DK.MWINYI  AWASILI DAR KUHUDHURIA UZINDUZI WA JUKWAA LA MTANDAO WA CHAKULA AFRIKA, AGRF 2023*

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi   ameondoka Zanzibar  leo na kuwasili Dar es Salaam kuhudhuria uzinduzi wa Jukwaa la Mtandao wa chakula Afrika  AGRF 2023, utakaofanyika Ikulu Dar es Salaam amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Amos  Makalla na viongozi wengine wa Mkoa huo.

📅 17 Machi, 2023

📍Terminal One, Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi mbalimbali wa D...
03/03/2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wa vyama vya Siasa kumsalia na kumwombea Marehemu Habib Ali Mohamed Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe katika Msikiti wa Masjid Zinjibar uliopo Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibia ambaye amefariki dunia leo Tarehe: 03 Machi. 2023. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wa vyama vya Siasa kumsalia na kumwombea Marehemu Habib Ali Mohamed Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe katika Msikiti wa Masjid Zinjibar uliopo Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibia ambaye amefariki dunia leo Tarehe: 03 Machi. 2023.

*SERIKALI IMEINGIZA BILIONI 32 KWA MAKUSANYO YA MWAKA UWANJA WA NDEGE ZANZIBAR*Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la ...
28/02/2023

*SERIKALI IMEINGIZA BILIONI 32 KWA MAKUSANYO YA MWAKA UWANJA WA NDEGE ZANZIBAR*

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kampuni zilizokuwa zikiendesha huduma za uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume kwa zaidi ya miaka 25, uwanja huo ulikuwa ukipata hasara pamoja na Serikali kulipa mishahara ya wafanyakazi wa uwanja huo. Baada ya kampuni ya Dnata kuanza kazi kwa mwezi wa disemba (robo ya mwisho wa mwaka) uwanja huo umekusanya Shilingi bilioni 8.1 ambapo wastani kwa mwaka ni shilingi bilioni 32.

Kwa upande wa makusanyo ya fedha za maegesho ya magari uwanja wa ndege ulikuwa ukipata shilingi milioni 2 ikilinganishwa na hivi sasa kwa mwezi wa januari Serikali imekusanya shilingi milioni 139.

Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar leo tarehe 28 Februari 2023.

*SERIKALI IMEINGIZA BILIONI 32 KWA MAKUSANYO YA MWAKA UWANJA WA NDEGE ZANZIBAR*Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la ...
28/02/2023

*SERIKALI IMEINGIZA BILIONI 32 KWA MAKUSANYO YA MWAKA UWANJA WA NDEGE ZANZIBAR*

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kampuni zilizokuwa zikiendesha huduma za uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume kwa zaidi ya miaka 25, uwanja huo ulikuwa ukipata hasara pamoja na Serikali kulipa mishahara ya wafanyakazi wa uwanja huo. Baada ya kampuni ya Dnata kuanza kazi kwa mwezi wa disemba (robo ya mwisho wa mwaka) uwanja huo umekusanya Shilingi bilioni 8.1 ambapo wastani kwa mwaka ni shilingi bilioni 32.

Kwa upande wa makusanyo ya fedha za maegesho ya magari uwanja wa ndege ulikuwa ukipata shilingi milioni 2 ikilinganishwa na hivi sasa kwa mwezi wa januari Serikali imekusanya shilingi milioni 139.

Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar leo tarehe 28 Februari 2023.

@

*DK.MWINYI AFUNGUA RASMI MADUKA YA DARAJANI SOUK*Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mw...
18/02/2023

*DK.MWINYI AFUNGUA RASMI MADUKA YA DARAJANI SOUK*

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amefungua rasmi Mradi wa Maduka 452 ya Kisasa ya Darajani Souk.

📅18 Februari 2023,

📍Maduka Darajani Souk,Wilaya ya Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Sweden Nchini Tanzani...
13/02/2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe.Charlotta Ozaki Macias, na Ujumbe wake waliofika Ikulu,Zanzibar kwa Mazungumzo .

📅13 Februari 2023,

📍Ikulu, Zanzibar .

*RAIS DK.MWINYI ASISITIZA UHARAKA WA UANZISHWAJI MAHKAMA YA RUSHWA NA  UHUJUMU UCHUMI ZANZIBAR*Rais wa Zanzibar na Mweny...
13/02/2023

*RAIS DK.MWINYI ASISITIZA UHARAKA WA UANZISHWAJI MAHKAMA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI ZANZIBAR*

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema uanzishwaji wa Mahkama maalumu ya rushwa na uhujumu uchumi itaisaidia Serikali katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi na rasilimali za umma.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi alieleza kufarijika kwamba tayari kamati ya wataalamu imeundwa kusimamia na kuratibu mchakato wa kuanzishwa kwa Mahkama hiyo

Ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar viwanja vya Mahkama Kuu ya Zanzibar, Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika maadhimisho hayo Rais Dk.Mwinyi amezindua Bendera na Nembo rasmi ya Mahkama ya Zanzibar na kupokea ripoti ya utendaji kazi wa Mwaka 2022.

Alisema Serikali itatoa kipaumbele kikubwa katika bajeti yake kwenye matumizi ya Tehama na uimarishaji miundo mbinu ya taasisi za Sheria nchini.

📅13 Februari 2023,

📍Viwanja vya Mahkama Kuu Zanzibar,Mkoa wa Kusini Unguja.

Address

Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dadani Investment Company Limited posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share