Fresh-Shamba

Fresh-Shamba Fresh-Shamba is limited company dealing with distribution of seeds, fertilizers, pesticides and processing, storage, and distribution of farm commodities.

New project. Msimu wa kilimo umeaza. Nitaendelea kushare picha za matukio katika msimu huu wa kilimo
16/11/2023

New project.

Msimu wa kilimo umeaza. Nitaendelea kushare picha za matukio katika msimu huu wa kilimo

31/12/2017

MUHIMU
Magonjwa ni chanzo kikuu cha vifo kwa kuku wa Asili na hii husababisha hasara katika ufugaji, hivyo basi:
1.Kinga ni bora kuliko tiba.
2.Fanya usafi wa mabanda yako ya kuku mara kwa mara.
3.Hakikisha vyombo vya chakula na maji ni visafi.
4.Toa lishe iliyokamilika na ya kutosha.
5.Pata ushauri wa mara kwa mara kutoka kwa wataalamu wa mifugo waliopo karibu na makazi yako.
6.Kuku wageni watengwe kwa muda usiopungua siku 14 kabla hawajachanganywa na kuku wenyeji na wapewe chanjo.

31/12/2017

KILIMO BORA CHA TIKITI MAJI (WATERMELON)

UDONGO NA JOTO

Usiwe wa kutuamisha maji
Ukiwa Tifutifu, AU kichanga Tifutifu (Clay loam) na hali ya joto kiasi angalau 15- 35 degree inatosha sana
Linahitaji maji mengi mwanzoni lakini kadri linavyoendelea maji unapaswa kupunguza

MUDA WA KUOTA

Ukisia mbegu huchukua siku 5 hadi 10 kuota

K**A SHAMBA LIKO TAYARI BY NOW, UKIPANDA SIKU 75 HADI 90 (AINA ZA MBEGU ZILIZOPO SOKONI KWA SASA NI HYBRID -ZEBRA, 1. SUKARI F1, 2. MSHINDI, 3. JULIANA ETC)

KWA TIKITI JITAHIDI SANA KUPANDA KWA NAFASI

K**A UTALIMA MATUTA BASI TUTA LIWE LIMEINUKA KIASI KUJA JUU WALAU SM 20 HIVI LIWE NA UPANA WALAU WA SM 45 HADI 60, UPANDAJI, KUTOKA SHIMO HADI SHIMO SM 90 HADI 100, NA KUTOKA KATIKATI YA TUTA HADI TUTA LINGINE NI MITA 1.5=SM 150, KWA HIYO KWA MATUTA YANAYOFUATANA TIKITI ZIIKIANZA KUTAMBAAA UNAZILAZA ZINAKUTANA KATIKATI YA HIZO TUTA MBILI

K**A UTAAMUA KUPANDA KWA MAJARUBA K**A HAYA YA MPUNGA, AMBAPO WATU WENGI HUMWAGIA KWA KUTENGENEZA MITALO YA KIENYEJI YA UMWAGILIAJI BASI, JARUBA LAKO LINAPASWA KUWA NA UPANA WA MITA 3 NA UREFU WOWOTE ULE HATA WA MITA 5 ILI MRADI UWEZE KUMUDU KUINGIZA MAJI.

SASA KWA JARUBA TUNAPANDA PEMBENI KATIKA ANGLE HIZO. KUTOKA SHIMO HADI SHIMO NI HIZO SM 90 (=futi tatu), AMBAPO SASA YAKIAANZA KUTAMBAA UTAYALAZIA KATIKATI HAPO KATIKA HUO UPANA WA MITA 3, SO YA KULIA YATAKUJA HAPO CENTRE, YA KUSHOTO , KASK, NA KUSINI HIVYO HIVYO YANAKUJA KULALA HAPO

MBOLEA ZA KUPANDIA NI MUHIMU SANA

UKIPATA YARA MILA WINNER ( NAMBA HIZI 15:9;20 AINA YA NPK) ITAKUFAA KILA SHIMO UNALOWEKA MBEGU MOJA WEKA GRAMA 10 YA MBOLEA SWA NA KIJIKO KIMOJA KIKUBWA CHA WALI. ZITAOTA BADA YA SIKU 5 HADI 10

AFTER ONE-THREE WEEKS TANGU KUOTA MBEGU, UTAWEKA MBOLEA YA KUKUZIA K**A CAN AU UREA (UREA UIWEKE BAADA YA KUWA UMEMWAGIA MAJI MENGI SHAMBANI)

MAUA YAKIJA JITAHIDI UPATE BOOSTER (HIZO NI MAALUMU KWA AJIRI YA MAUA NA MATUNDA

ZIPO BOOSTER ZINAITWA STAARTER- MFANO HALISI ZILIZOPO MADUKANI NI POLYFEED STARTER-HIZO HUTUMIKA KUPIGA MAUA WAKATI WA MAUA

MATUNDA YAKIJA UTAWEKA POLYFEED FINISHER-HIYO NI KUIMARAISHA MATUNDA, NA PIA UTAFUTE MBOLEA INAITWA YARA NITRABOR (HII INA Calcium na Nitrojen kwa wingi) , husaidia kuzuia tikiti kunyauka, na kuzoa katika kitako-Ugonjwa unaitwa Blosom End Rot

WAKATI WOOTE WA MAISHA YA TIKITI USISAHAU DAWA ZA WADUDU, WANAOKATA MAUA , NA KUTOBOA MATUNDA, DAWA K**A DUDU ALL AU SELECRON, AU MATCH, AU KARATE MOJA WAPO YATOSHA KUMALIZA WADUDU

LAKINI WAKATI WA KUPIGA HIZI DAWA KUWA MAKINI SANA USIPIGE MCHANA, UTAUWA NYUKI WA KUFANYA UCHAVUSHAJI KUTOFANYIKA-HAPO UTAPATA DIFORMALITIES NYINGI SANA K**A SHAPELESS KATIKA MATUNDA, PIGA ASUBUHI SANA AU JIONI SANAA,

PIA K**A UTAONA KUNA HALI YA UKUNGU (UNYEVU NI MWINGI AU BARIDI USIKU AU MCHANA) NI MUHIMU KUWEKA DAWA ZA JAMII YA COPPER, K**A BLUEE COPPER, AU EBONY KUZUIA UKUNGU,

NI MUHIMU SANA KUHAKIKISHA TIKITIKI ZAKO ZINAPATA MAJI WALAU MARA 3 KWA WIKI, ILI KUPUNGUZA WATER SRESS

GHARAMA ZA MBEGU

KWA EKARI MOJA UTAHITAJI Gram 300 za mbegu , ambapo jumla ya gharama za mbegu ni kati ya tsh 200,000 hadi tsh 300,000

MAVUNO

Kwa nafasi tajwa hapo juu utakuwa na mashimo yasiyopungua katiya 2000 hadi 3000 Kwa ekari moja. Hivyo kila shimo au kila kamba ya tikiti ikikupa matikiti matatu means utakuwa na mavuno ya vichwa vya tikititi kati ya 6000 hadi 9000, ambayo ni sawa na wastani wa tani 12 hadi 18 kwa ekari moja. Zidisha kwa bei iliyopo sokoni.
Ukiwa na dhamira ya kweli mafanikio kupitia kilimo yanawezekana.

31/12/2017

Kumbukumbu
Mfugaji anashauriwa atunze kumbukumbu za chanjo na matibabu ili zimsaidie kujua yafuatayo:
- Muda sahihi wa kuanza chanjo na kurudia chanjo.
- Idadi ya kuku wanaotakiwa kuchanjwa muda wa kuchanja ukifika.
- Kiasi cha dawa kinachohitajika (dozi) kuandaliwa.
- Aina ya chanjo inayohitajika kulingana na magonjwa yanayojitokeza mara kwa mara.

Kushirikiana
Udhibiti wa magonjwa kwa njia ya chanjo unahitaji nguvu ya pamoja ili kupata matokeo mazuri. Ni vizuri wafugaji kwenye eneo moja wakishiriki kupanga mkakati na kusimamia utekelezaji wa suala zima la uchanjaji. Umuhimu wa kuchanja kuku kwa wakati mmoja katika eneo ni muhumu ili kudhibiti ugonjwa kwa wakati mmoja. Mfugaji anayeamua kuchanja azingatie ratiba ya chanjo ya ugonjwa husika ili kuweza kupata matokeo mazuri.

SHARE NA MARAFIKI

31/12/2017
31/12/2017

MATUNZO YA KUKU ANAE ATAMIA MAYAI.

Wafugaji wengi hawajali sana mazingira mayai yalipo ya kuku anayeatamia wakidhani kuku mwenyewe atafanya kila kitu. Makala hii inakupa elimu ya nini cha kufanya kwenye eneo analotagia kuku na wakati wa kuatamia. Futana nami kwenye makala hii fupi.

Kuku wanaotazamiwa kuatamia lazima wachunguzwe kwa makini kwa siku mbili kabla ya kuatamia ili kuhakikisha hawana chawa, utitiri au viroboto. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na wasitulie katika viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa vifaranga wachache au kutoanguliwa kabisa kwa vifarnga na kuishia kupata mayai viza. Ikiwa kuku kwa namna yeyote ile kuku au eneo wanaloatamia lina wadudu hao basi nyunyizia dawa ya kuua wadudu hao. Nenda kwenye maduka ya mifugo ukanunue dawa ya kuua wadudu hao.
Kuku kwa ajili ya kuatamia awe na histori ya tabia ya kuangua vifaranga wengi. Hivyo uwe na tabia ya kuwachunguza kuku wako kujua ni kuku yupi anafaa kwa kuatamia kati ya kuku ulionao.

Kwa baadhi ya wafugaji hutumia mashine za kutotolesha vifaranga au kupeleka mayai kwa wenye mashine hizo ili wakatotoleshe mayai ya kuku wao. Baadhi ya wafugaji walio kijijini hii huwa ni changamoto kwani upatikanaji wa mashine hizo huwa si rahisi. Hivyo wengi hutumia ule mfumo wa kumnyan’ganya kuku vifaranga na kumuekea mayai mengine ili aendelee kuatamia. Mfumo huu ni mzuri ila humdhofisha sana kuku yule ambaye yupo kwa ajili ya kuatamia.

Ni kweli kuwa kuku anaetaga hatakiwi kupewa vyakula vitakavyo mfanya awe na mafuta sana. Kwani kuku anaetaga akiwa na mafuta sana hupunguza kutaga au kuacha kabisa.

Wafugaji wengi, kuku punde aanzapo kuatamia husahau kuwabadilishia mfumo wa chakula na utaratibu wa kuwalisha. Kuku anae atamia hasa yule ambaye akitotoa anawekewa mayai mengine chakula chake kinatakiwa kiwe na virutubisho vyote wanga, madini na protini ili kumfanya awe na nguvu ya kuendelea kuatamia bila kudhoofika . Ni vema kuku wanao tumiwa kuatamia wawe wanapumzishwa, unaweza kuamua wewe mwenyewe kuwa kuku wako aatamie mala ngapi baada ya hapo unampumzisha. Pia kuku wanao atamia inatakiwa chakula na maji viwe kalibu na kiota chake ili asipate usumbufu kufata chakula. Ni vizuri kuwa sehemu salama na tulivu ambayo kuku wengine hawata msumbua au kupasua mayai. Sehemu anapo atamia kuku hakikisha kuwa mvua ikinyeesha hapavuji. Ikitokea kuku wengine umewapa chanjo basi usimsahau na yeye kumpa hiyo chanjo. Kuku anae atamia anahitaji uangalizi mkubwa kwani usipo kuwa makini nae anaweza pata ugonjwa bila wewe kujua, nakuja kufa gafla.

Hizi ni baadhin ya dondoo muhimu kwa mfugaji wa kuku ili kuongeza uzalishaji wa vifaranga.

31/12/2017
31/12/2017



KILIMO BORA CHA NYANYA

LIMA SASA KWANI BEI YA NYANYA INAYOINGIA SOKONI KUANZIA DISEMBA HADI MARCH BEI KWA CRET HUWA TShs 60,000-80,000.

AINA
Ziko nyingi k**a fupi kiasi (Semi Determinent), k**a-AINA HIZI HUWEZA KUVUNA KWA MIEZI 2 HADI 4 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA

A; Semi-determinent

1. Eden (Hii inafaa sana wakati wa mvua nyingi-Ni imara dhidi ya ukungu,/Baridi)
2. Ipo Shanty
3. Assila-Hii ni imara sana wakati wa Ukame
4. Kipato-

B; Aina Ndefu (Indeterminent)-AINA HIZI NDEFU HUWEZA KUVUNWA MFULULIZO KWA MIEZI 8 HADI 12 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA)-HUWEZA KUREFUKA HADI MITA 5 KWENDA JUU

AINA HIZO NI 1. ANNA F1 2. COLAZON 3.DIVINE 4. GALILEYA 5. EVA

C; AINA ZA OPV-OPEN POLLINATED VARIETIES
1. RIo Grande
2. Onyx
3. Tengeru 97
4.Mkulima

MAZINGIRA
i. Joto la kadri 20-35 degree sentigrade

ii. UDONGO
-usituamishe maji, Kichanga tifutifu utafaa zaidi, Wakati wa kupanda ukipandia samadi au mboji itafaa zaidi ili kuimarisha udongo

iii. NAFASI YA KUPANDA

-Ni vizuri ukatengeneza matuta ya upana japo wa sm 60, na ukapanda double line (Mistari miwili katika tuta moja) nafasi ndani ya mstari ni sm 60 kwa 60 na umbali kati ya mstari na mstari ni sm 45, LAKINI k**a utapamda mistari miwili ndani ya tuta moja (raised bed) hakikisha mche wa kwanza katika mstari wa pili unakuwa upo katikati ya miche miwili ya mstari wa kwaza ili KUPATA ZIG ZAGA SHAPE

-Umbali wa tuta hadi tuta,
Umbali wa kutoka katikati ya tuta moja hadi jingine liwe ni 1.5 MITA

Njia hii ya matuta ni nzuri sana k**a utaweka drip line (Drip Irrigation)

K**a hauna drip, basi tengenza matuta lakini pande pembeni mwa tuta (chini kidogo mwa tuta) maana kwa njia hiyo utamwagia kwa njia ya Furrow (Mifereji)

Upandaji maarufu ni sm 60×60 mche mpaka mche na mstari mpaka mstari

KIASI CHA MBEGU
kwa ekari moja utahitaji Mbegu gram 100-150 kwa OPV variety, na Gram 30-50 kwa hybrid (F1) . Gharama za kutosha eka moja kwa OPV variety ni tsh 100,000-180,000, na kwa Hybrid (F1) Gharama ni kati ya tsh 200,000-400,000 kutegemea na aina yenyewe ya mbegu.

UPANDAJI

Sia mbegu katika kitalu, tengeneza tuta la upana wa mita moja hadi mbili, na urefu wowote utakao, na kisha chora vimifereji vidogo vidodgo kwa kijiti, vilivyoachana baina yake kwa sm 5, kisha dondosha mbegu taratibu, na kisha fukia na layer ndogo ya mchanga, kisha weka nyasi kavu na mwagia maji, hakikisha unamwagia maji uliyochanganya na DAP MBOLEA, Gram 100 sawa na UKUBWA WA KIGANJA CHAKO KIMOJA, WEKA KATIKA MAJI LITA 15/20 KISHA MWAGIA KWA KILA TUTA.

Maji yamwagiwe angalau kwa siku mara mbili (SAA 2 ASUBUHI NA SA 11 JIONI)

MBEGU ZITAOTA BAADA YA SIKU 7 HADI 10 tangu kusia mbegu.

ZIACHE MBEGU KATIKA KITALU KWA MUDA WA WIKI 3 TU KISHA HAMISHIA SHAMBANI.

MAMBO YA KUFANYA SHAMBANI

Kabla ya kupandikiza hakikisha kitalu kimemwagiwa maji ya kutosha-ili iwe rahisi kung’oa miche, na shamba pia liwe limemwagiwa vya kutosha.

-hakikisha umechimba mashino mashimo yako kwa nafasi, na kisha kila shimo lipate angalau gram 10 hadi 20 za mbolea moja wapo ya hizi (Yara Miller winner, TSP, DAP, AU Minjingu au NPK)

Kisha weka mmea wako na fukia vizuri udongo, siku hiyo baada ya kupandikiza hakikisha kila mmea unapata angalau ml 250 za maji

BAADA YA KUPANDIKIZA

Chunguza sana juu ya wadudu, wakatao shina (Cutworm), pamoja na wale wanaoharibu majani

Dawa k**a Karate, Duduall, Match, Selecron, moja wapo itakufaaa kukabiliana na wadudu hao

Baada ya siku 15 tangu kupandikiza weka mbolea ya kukuzia moja wapo ya hizi, CAN, Yarra miller winner, au Hata NPK,

Baada ya siku 25 tangu kupandikiza miche itaanza kutoa vitunda vya maua, Hapo unahitaji booster za majani na maua (KUZUIA MAUA YASIDODNDOKE) k**a vile, Polyfeed starter, au Multi K (19:19;19), au Yara Miller Tracel Biz AU Wauxal Macro Mix

WAKATI HUU WA MAUA NI MUHIMU

Kuzingatia dawa za kuua wadudu, zipigwe asubuhi sana au jioni sana, ukizipiga mchana saa 6 hadi saa 9, utaua nyuki (watakimbia) na matunda yatajitengeneza bila fertilization, yatakuwa seedless au shapeless

MATUNDA YAKIJA

Ni muhimu kuzungusha chini katika mizizi mbolea ya Yara Nitrabo, au yoyote yenye Calcium, ili kuzuia kuoza kwa kitako cha matunda (Blosom End rot), au matunda kupasuka-Cracking

WADUDU
Wadudu wasumbufu wa nyanya, ni funza wa matunda, wanaokata miche michanga, wadudu wanaoscratch majani. Leaf miner (Wachora ramani katika majani)

Magonjwa

Kinyaushi cha kwanza, (Early Bright), Kinyaushi cha mwisho (ate Bright), magonjwa ya bakteria na ukungu(Unga mweupe katika matunda), Baka jani (Leaf spot)

MUDA WA KUKOMAA
NYANYA HUCHUKUA KATI YA SIKU 90 HADI 120 TANGU ZILIPOSIWA KATIKA KITALU HADI KUKOMAAA

MAVUNO

Ekari moja inaweza kutoa cret 1300 za kilo 50, sawa na tani 35

SOKO

Nyanya yenye bei nzuri ni ile ya inayoingia sokoni kuanzia disemba hadi March-Nyakati hizo bei kwa cret moja hufika hadi tsh 80,000

NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, K**A SASA KUNA MDUDU ANAITWA Tuta Absoluta.. au waswahili wanamuita KANITANGAZE (MAANA AKIKUVAMIA SHAMBANI HAKUNA NAMNA UTAACHA KWENDA KUMSIMULIA) Anakausha matunda, na kuyaozesha pamoja na kusababisha matunda kudhoofika.CHANGAMOTO KUBWA WASIYOIJUA WAKULIMA NI KUWA DAWA ZA KUZUIA MDUDU HUYU INABIDI ZIPIGWE KUANZIA MCHE UNAPOKUWA KATIKA KITALU..

WENGI WA WAKULIMA HUKIMBIZANA KUTIBU MDUDU HUYU WANAPOONA MATUNDA YAMEVAMIA (YAMEOZA, AU YAKO NA MAKOVU KATIKA KISHIKIO Calyxn)
LAKINI DAWA DHIDI YA MDUDU HUYO ZIPO KWA SASA

DAWA ZA KUTUMIA
1. Colagen,na Belt (Hizi lazima uzitumie alternatively, wiki hii unapiga Belt wiki ijayo unapiga Colagen) Ukitumia moja tu hautafanikiwa, maana Colagen inaweza kuua zaidi mayai na yule funza, na Belt inamafanikio zaidi katika kuua yule mother kipepeo mwenyewe. Dawa hizo ni za kampuni ya Buyer (Waingereza/Wajerumani)

2. Nimbecidin-Ni dawa ipo kwa sasa inafanya vizuri, asili yake ni mafuta ya Mwarobain (Neem)
3. Evisect-Inasambazwa na Arysta Life Science inafanya vizuri
4. Abamectini au Dyinamec pia inafaaa sana

Address

Tabora

Telephone

0789691969

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fresh-Shamba posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share