UDA Rapid Transit - UDART

UDA Rapid Transit - UDART UDA Rapid Transit PLC
Tumejikita katika kutoa huduma za usafirishaji wa abiria katika jiji la Dar es Salaam na Pwani

07/04/2026
UDART YAUNGANA NA WATANZANIA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANIKampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) imeungana na...
09/03/2026

UDART YAUNGANA NA WATANZANIA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) imeungana na Watanzania na jumuiya ya kimataifa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, kwa kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya jamii na sekta ya usafiri.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika tarehe 08 Machi 2026, yamewakutanisha wafanyakazi wa UDART wakiwemo wanawake wanaofanya kazi katika nyanja mbalimbali ndani ya kampuni hiyo k**a vile uendeshaji wa Mabasi, huduma kwa wateja, uhandisi pamoja na utawala.

Uongozi wa UDART umeeleza kuwa kampuni inaendelea kuthamini na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika sekta ya usafiri wa Umma, huku ikisisitiza kuwa wanawake ni nguzo muhimu katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, UDART imeendelea kupongeza juhudi za wanawake wote wanaofanya kazi katika Kampuni ya UDART kwa kujituma na kuchangia maendeleo ya huduma za usafiri wa Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.

Kupitia maadhimisho ya mwaka huu, UDART imeahidi kuendelea kuweka mazingira rafiki ya kazi kwa wanawake pamoja na kutoa fursa sawa za ajira, mafunzo na maendeleo ya kitaaluma ili kuongeza ufanisi na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hufanyika kila mwaka tarehe 8 Machi na hulenga kutambua mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo pamoja na kuhamasisha usawa wa kijinsia duniani.

2026 UDART tuko tayari kukuhudumia ๐Ÿ™
08/03/2026

2026 UDART tuko tayari kukuhudumia ๐Ÿ™

06/02/2026
UDART YASHIRIKI KIKAO KAZI CHA NAIBU WAZIRI TAMISEMIKampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) imeshiriki katika Kikao Ka...
26/01/2026

UDART YASHIRIKI KIKAO KAZI CHA NAIBU WAZIRI TAMISEMI

Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) imeshiriki katika Kikao Kazi maalum kilichoitishwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu โ€“ TAMISEMI Mhe. Reuben Kwagilwa (Mb) tarehe 24 Januari 2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Millenium Tower Jijini Dar-es-Salaam kuanzia majira ya saa nne asubuhi.

Kikao hicho kililenga kujadili mikakati ya uimarishaji wa Kampuni ya UDART, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya TAMISEMI na Taasisi ya UDART kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za usafiri wa Umma ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri wa TAMISEMI aliahidi kuisimamia vyema Kampuni ya UDART na kuhakikisha inaimarishwa kiutendaji, kifedha na kimkakati ili kuongeza ufanisi wa huduma za usafiri wa Umma na kukidhi mahitaji ya wananchi.

Mhe. Naibu Waziri wa TAMISEMI pia alionesha umuhimu wa kuwepo kwa Kampuni ya Serikali katika Sekta ya Usafiri wa Umma kwakuwa inakamilisha dhana ya uzalendo wa Serikali kaika utoaji huduma kwa kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake, Uongozi wa UDART ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Ndg. Pius Andrew Ngโ€™ingo uliwasilisha Taarifa ya hali ya utekelezaji wa majukumu ya kampuni, mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zilizopo, na kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kuimarisha zaidi kampuni kupitia ushirikiano wa karibu na Serikali na wadau wengine.

Kikao hicho kimeonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuhakikisha UDART inaendelea kuwa mhimili muhimu wa maendeleo ya mfumo wa usafiri wa Umma na kuchangia ustawi wa wananchi.

UJIO MPYA NA HUDUMA BORA ZAIDI UDARTDar es salaam, baada ya kupokea Mabasi 49 CNG na pia kusubiri Mabasi 50 mengine yana...
19/01/2026

UJIO MPYA NA HUDUMA BORA ZAIDI UDART

Dar es salaam, baada ya kupokea Mabasi 49 CNG na pia kusubiri Mabasi 50 mengine yanayotarajiwa kuwasili 28/01/2026, taratibu za mpangilio wa kihuduma zinaendelea ili kuhakikisha Watanzania wanapata vyema huduma za usafiri kwa Usalama ,Uhakika na Haraka zaidi.

2026 UDART TUKO TAYARI KUKUHUDUMIA.

Address

Jangwani
Jangwani

Opening Hours

Monday 05:00 - 23:00
Tuesday 05:00 - 23:00
Wednesday 05:00 - 23:00
Thursday 05:00 - 23:00
Friday 05:00 - 23:00
Saturday 05:00 - 23:00
Sunday 05:00 - 23:00

Telephone

+255652030233

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UDA Rapid Transit - UDART posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to UDA Rapid Transit - UDART:

Share