07/08/2023
UHUSIANO WA AKILI NA MAVAZI
Marko 5:15
[15]Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.
Kwenye huu mstari tunakutana na habari ya mtu aliyekua kichaa kwa sababu ya pepo na alikua havai nguo kabisa.
Alipofunguliwa na Yesu akawa na akili zake , walimkuta pia amevaa nguo zake.
Kwa hiyo
"Kiwango cha mwili unachokiacha wazi kinatuonyesha kiwango cha akili ulichonacho. Anayetembea uchi kabisa hana akili kabisa, anayetembea nusu uchi ana akili nusu pia"
Pastor Francis Langula
(RETREAT CAMP OF AUGUST 2023)