M&J DSM Company LTD

M&J DSM Company LTD M & J DAR ES SALAAM COMPANY LIMITED

Dealing With:
• Clearing & Forwarding
• Film & Video Production
• Marketing & Advertising
• Tourism & Tour Operations
• Car Hire
• Hotel Booking
• Event Management
• Promotions
• Cleaning & Fumigation Services
• Secretarial Services

24/08/2016
27/02/2016

Kipindi utakapokubali kutoka kimapenzi na mme wa mtu, utakuwa umekubaliana kuwa mwanamke wa daraja la pili. Na s*ku zote mtu wa daraja la pili ni mtu wa daraja la chini ukilinganisha na daraja la kwanza.

Angalia sasa...k**a yupo na wewe na mke wake akapiga simu atamdanganya mkewe kwamba yupo ofisini au katika kikao na hautakuwa na ujasiri wa kuingilia mawasiliano yake. Pia anapokua nyumbani kwake kwa mkewe huwezi kumpigia au hata kumtumia text.

Dada yangu wewe ni mdoli? Anakuchukua kwenu na gari yake anakupeleka katika vyumba vya hotel lakini mke wake amemkabidhi nyumba nzima. Dada yangu shtuka!!

Anakutembelea nyumbani kwako na unamtambulisha kwa rafiki zako na majirani kwamba ni boyfriend wako bila kujua unajizibia nafasi za kupata mtu sahihi wa kuweza kujenga nae maisha. Na mbaya zaidi hupajui hata yeye anapoishi.

Dada yangu mpaka lini utaendelea kujiharibia future yako? Anatoka na wewe out na anakununulia kila aina ya pombe na wakati huo huo hawezi kumruhusu mkewe kunywa pombe ya aina yoyote ile. Akili ya kawaida ikwambie kwamba anafanya hivyo ili ulewe vilivyo na apate wasaa wa kukukandamiza vizuri kitandani.

Dada yangu Je mwili wako ni wa majaribio? Anakupa mimba na anakupa pesa uende ukaitoe lakini mke wake akipata mimba nyumbani ni sherehe na anampa pesa za kuandaa martenity dress na vitu vya mtoto.

Dada yangu kumbuka tayari anayo familia yake, k**a ulikua hujui Jamaa huwaelezea marafiki zake yote mnayofanya hotelini, lakini hata s*ku moja hawezi kuwalezea yale anayofanya na mkewe. Hii inafanya marafiki zake wakuone k**a mwanamke wa hadhi ya chini kabisa.

Unazo picha zake katika simu yako na ume save namba yake kwa majina mazuri k**a Sweetheart, My love, etc... Lakini picha zako haziwezi kupatikana ktk simu yake na namba yako amei Save k**a Fundi Genereta, Fundi gari, Mzibua Chemba.

Unatakiwa ukumbuke kwamba mwanamke asie na akili sehemu zake za siri ndizo zitakazoumia zaidi.

Amka dada yangu unatumika

16/02/2016

WATOTO ZETU TWISHENI YA MALEZI NA LUNINGA a.k.a KIOO a.k.a KIDEO

Luninga aka TV aka
a.k.a KIOO a.k.a KIDEO, kinadanganya watu ni kitu moja hatari sana. Siku hizi TV ndio imekuwa shule ya kila kitu. Kuvaa, kuongea, kuimba, kucheza, na s*ku hizi mpaka kulea.

Wasanii wanatengeneza video za singo zao kwa kukopi na kupest zile walizoona kwenye Luninga, hata muvi zinatengenezwa baada ya wajanja wetu kuangalia muvi kwenye Luninga, kisha kukopi na kupesti za kwao. Ila kali sasa ni wale jamaa zangu wanakopi na kupesti namna ya kulea watoto wao kwa kujifunza kwenye luninga.

Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi k**a wale anaowaona kwenye Luninga, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea k**a vile vitoto vya kwenye Luninga, mwenyewe anakaita Gunia sijui junia ndio hivyo hivyo, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote.

Nilipata taarifa kuna s*ku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, "No Junia no...! is bad!” Na kucheka cheka huku akisifu, "Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei s*ku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, "Junia no!", anapanda meza mara kabati, jamaa yangu na mke wake utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, "No Junia no" Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, 'Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, 'No Junia no'.

Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Junia akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi...! "Leo umekuja kula kwetu?" "Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?" Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, "Junia yu a veri bed". Sasa chenyewe si kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii dharau.

Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho k**a kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichini... "We Junia ukinisogelea tena nakukata mas*kio kabisa".

Eeh bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza "Junia umefanya nini tena baba?" kimya "Junia what has happened?" kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake, "Huyu kafanya nini?" Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa... "Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko".

Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, "Junia a yu s*k? Unaumwa?" Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa mas*kio.

Wengine hatuangaliagi Luninga ohooo!

23/01/2016

・・・
Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi
wakafanya mazungumzo. Mmoja aling'ang'nia
kuzungumzia kero za familia yake hatimaye
mwenzake akasema " Unadhani familia yako ina
matatizo?" Basi s*kiliza kisa changu hiki….
"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke
mjane aliyekua na binti mkubwa tu na mimi na
huyo mjane tukaamua kuoana. Baadaye baba
yangu akamuoa binti yangu wa kambo (yaani binti
wa huyu mke wangu niliyemwoa akiwa mjane),
hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama
yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto
wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu
akawa mama mkwe wa mkwe wake.
Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa
kambo (ambaye kwa sasa ndiye mke wa baba
yangu na hivyo kuwa pia mama yangu wa kambo)
alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume
akawa mdogo wangu kwa sababu tulichangia baba
mmoja. lakini kwa vile pia alikua ni mtoto wa binti
wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke
wangu na mimi nikawa babu yake huyo mdogo
wangu.
Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na
mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa
msichana (yaani binti ya mke wangu ambaye pia ni
mke wa baba yangu) ambaye ni ndugu wa mtoto
wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao
mmoja, akawa pia bibi yake na mwanangu
(mwee!!). Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kuwa
shemeji wa mtoto wangu (achilia kuwa babu
yake!!) ambaye ndugu yake wa k**e kwa upande wa
mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo
mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo
ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa
binti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni
mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu
yangu mwenyewe...
🙈🙈🙈

14/05/2015

Jeshi la polisi Mkoani Simiyu linamshikilia Chigila Gilala mkazi wa kijiji cha Bukigi kata ya Malampaka wilayani Maswa (45) kwa kosa la kukutwa na viungo zinavyodhaniwa kuwa vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa.Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM katika kijiji hicho na Mganga wa tib

26/12/2014

Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza

22/12/2014
22/12/2014
18/11/2014

Waziri wa Afya Mhe.Dkt Seif Rashidi aongoza zoezi la kupima afya za Wabunge katika Ukumbi wa Msekwa jana.Upimaji wa afya za Wabunge umefanywa na Madaktari wa Aga Khan ku

11/10/2014
17/09/2014

Aunty akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani s*ku ya Jumanne Sept 16, 2014. Aunty Ezekiel akipata picha ndani ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania Washington, DC Aunty akipata picha nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.

Address

P. O BOX 75145
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when M&J DSM Company LTD posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to M&J DSM Company LTD:

Share