Christopher & Diana Mwakasege(Mana Ministry)

Christopher & Diana Mwakasege(Mana Ministry) Yohana 21:17.......Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.

14/04/2026
Kuombea Akili kwa Wiki 52 ili Zifanye Kazi Ipasavyo na Imani yako.Kitabu ni tshs 10,000Kitabu kinapatikana ofisi ya Dar ...
14/04/2026

Kuombea Akili kwa Wiki 52 ili Zifanye Kazi Ipasavyo na Imani yako.
Kitabu ni tshs 10,000
Kitabu kinapatikana ofisi ya Dar es salam jengo la Luther House ghorofa ya 3 (Kanisa la Azania Front) 0742 525225
Arusha ofisi ya mjini karibu na ofisi za Tanesco 0736 501081
Kwa wanaohitaji kitabu hiki nje ya mikoa ya Arusha na Dar es salaam,piga simu 0736 501081.
Mungu awabariki sana!

KITABU KIPYA!!“Mambo ya Kufanya Unapokataliwa na Mifumo Kimfumo”10,000tshsKitabu kinapatikana ofisi ya Dar es salaam jen...
14/04/2026

KITABU KIPYA!!
“Mambo ya Kufanya Unapokataliwa na Mifumo Kimfumo”

10,000tshs

Kitabu kinapatikana ofisi ya Dar es salaam jengo la Luther House ghorofa ya 3 (Kanisa la Azania Front) 0742 525225
Arusha ofisi ya mjini karibu na ofisi za Tanesco 0736 501081.
Kwa wanaohitaji kitabu hiki nje ya mikoa ya Arusha na Dar es salaam,piga simu 0736 501081.
Mungu awabariki!

“Unavyoweza Kupokea Uponyaji Wakati Unashiriki Chakula cha BWANA”. Kitabu ni shs 10,000.Kitabu hiki kinapatikana Ofisi z...
13/04/2026

“Unavyoweza Kupokea Uponyaji Wakati Unashiriki Chakula cha BWANA”.
Kitabu ni shs 10,000.
Kitabu hiki kinapatikana Ofisi zetu za Dar es salaam 0742 525225 jengo la Luther House ghorofa ya 3.
Ofisi za Arusha Mjini 0736 501081 karibu na ofisi za tanesco
Kwa wanaohitaji kitabu hiki nje ya mikoa ya Arusha na Dar es salaam,piga simu 0736 501081.
Mungu awabariki!

11/04/2026

Bwana Yesu Asifiwe!
Tunawakaribisha kwenye semina ya neno la Mungu, DODOMA Mjini katika UWANJA WA WAJENZI,nyuma ya kituo cha mafuta cha puma. Semina inaanza tarehe 15/4/2026 hadi 19/4/2026, kwanzia saa 9 alasiri hadi saa 12 jioni. Semina itarushwa LIVE Youtube kwenye channel yetu,Upendo TV na redio mbali mbali. Mungu awabariki.

“Hekima za Kibiblia za Kuweka Akiba ili Uepukane na Umasikini.”Ni shs  10,000Kitabu hiki kinapatikana ofisi zetu za Dar ...
09/04/2026

“Hekima za Kibiblia za Kuweka Akiba ili Uepukane na Umasikini.”
Ni shs 10,000

Kitabu hiki kinapatikana ofisi zetu za Dar es salaam 0742525225 jengo la Luther House ghorofa ya 3
Ofisi za Arusha mjini 0736501081karibu na Ofisi za Tannesco
Kwa wanaohitaji kitabu hiki nje ya mikoa ya Arusha na Dar es salaam, piga simu 0736501081.
Mungu awabariki sana!

04/04/2026

UJUMBE WA PASAKA 2026
TOKA KWA CHRISTOPHER MWAKASEGE
“Yesu akukumbuke leo katika ufalme wake”
Hili ni ombi ambalo, nimemwombea kila mtu anayepata nafasi ya kuusoma ujumbe wangu huu wa Pasaka. Ombi hilo ninalokuombea kwa Mungu ni hili: “Yesu akukumbuke leo katika ufalme wake”.
Ndiyo! Yesu akukumbuke leo, katika ufalme wake! Nimekuombea ombi hili, kwa sababu, “msalaba” ni lango kubwa sana la kiroho. Ni lango la kiroho, ambalo pia linaweza likakufungulia matokeo yake, katika ulimwengu wa kimwili.
Kufuatana na Wagalatia 3:13, msalaba uliwekwa k**a lango la “laana”. Lakini, tunaona ya kwamba, Yesu alisulubiwa msalabani, ili atubebee adhabu yetu. Adhabu hiyo ilitustahili sisi wanadamu, kwa sababu ya uasi wetu kwa Mungu.
Lengo kubwa mojawapo la Yesu kusulubiwa msalabani, lilikuwa ni Mungu kuutumia Msalaba, k**a lango la kumpa fursa kila amwaminiye Yesu, apate kupokea Baraka zake kiagano. Hii ni kufuatana na Wagalatia 3:14.
Siku ile Yesu aliposulubiwa, walisulubiwa pia wahalifu wawili – kila mtu katika msalaba wake binafsi. Ukiisoma habari hii katika Luka 23:32, 39 – 43, utaona ya kwamba, mhalifu mmoja aliitumia vizuri fursa ya lango la msalaba. Lakini, mhalifu mwingine, aliitumia vibaya fursa ya lango la msalaba!
Mhalifu aliyeshindwa kutumia vizuri fursa ya lango la msalaba, alijikuta anamsemesha Yesu maneno ya kumkebehi, na kuikebehi fursa ile ya msalaba iliyokuwa mbele yake. Biblia inasema: “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu” (1 Wakorintho 1:18).
Mhalifu aliyeitumia fursa ya lango la msalaba vizuri alimwomba Yesu akisema: “Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako” (Luka 23:42). Na Yesu akampa Mhalifu yule alichoomba (Luka 23:43).
Yesu yuko hai! Na tena, ndiye mfalme wa ufalme wa mbinguni (Wakolosai 1:13, 14).
Ni jambo gani unalotaka Yesu akusaidie, toka kwenye baraka za ufalme wake katika Pasaka hii ya mwaka huu?
Ni maombi yangu kwa Mungu, ya kuwa, utaitumia vizuri fursa ya lango la msalaba mwaka huu, ili kile ambacho Yesu atakupa toka katika ufalme wake, kikupe kumbukumbu nzuri katika maisha yako, tena iwe ya kudumu!
Ndiyo maana, nakuombea katika Pasaka hii, ya kwamba: Yesu akukumbuke leo, katika ufalme wake, kwa kukupa unachomwomba kwenye Pasaka hii!
Mimi na mke wangu, na familia yetu; na Timu nzima ya Huduma ya Mana, tunakutakia Pasaka njema, na yenye baraka!
Usisahau kumshirikisha na mwingine ujumbe huu, ili apokee na maombi yaliyomo ndani yake.

Mikakati 7 ya kuujenga Ufalme wa Mungu kwa njia ya Maombi.Kitabu ni tshs 10,000Kitabu kinapatikana ofisi ya Dar es salaa...
26/03/2026

Mikakati 7 ya kuujenga Ufalme wa Mungu kwa njia ya Maombi.

Kitabu ni tshs 10,000
Kitabu kinapatikana ofisi ya Dar es salaam jengo la Luther House ghorofa ya 3 (Kanisa la Azania Front) 0742 525225
Arusha ofisi ya mjini karibu na ofisi za Tanesco 0736 501081.
Kwa wanaohitaji kitabu hiki nje ya mikoa ya Arusha na Dar es salaam,piga simu 0736 501081.
Mungu awabariki sana!

Address

P O Box 2166
Arusha

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255739501081

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Christopher & Diana Mwakasege(Mana Ministry) posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Christopher & Diana Mwakasege(Mana Ministry):

Share